Hizi
ndizo Jezi mpya za timu za taifa zilizozinduliwa hii leo, kutoka
kushoto ni ya mazoezi nyumbani, inayofuatia ni ya nyumbani nyingine ni
ya ugenini na ya mwisho ni ya mazoezi ugenini.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa,
zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali
itakayokua inazikabili.
Uzinduzi
huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la
Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho,
uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika
uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini,
jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
No comments:
Post a Comment