Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Elius Maguri amesema hadi sasa hajajua sababu rasmi ya kuachwa na wekundu hao wa Msimbazi.
Kwa
mujibu wa Maguri, amekuwa akituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa
viongozi wa Klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapigia simu kutaka kujua
hatma yake, lakini hapati majibu.
Maguri
amefafanua kwamba walipotoka Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki
mbili , wachezaji walitakiwa kuingia kambini kujiandaa na mechi ya Simba
Day dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda, lakini jina lake halikuwepo.
Taarifa za chini zinaeleza kwamba Simba inataka kumtoa kwa mkopo au kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja kwasababu hayupo kwenye mipango ya kocha Dylan Kerr.
MABINGWA
wa zamani wa Afrika, TP Mazembe, wanatarajiwa kutua nchini kesho ambapo
pamoja na mambo mengine, watawachunguza kwa karibu zaidi nyota kadhaa
waliotamba kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika wiki
iliyopita jijini Dar es Salaam, wakiwamo Geoffrey Mwashiuya na Malimi
Busungu wa Yanga.
Kwa mujibu wa habari
zilizolifikia gazeti la BINGWA juzi, miamba hiyo ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC), imeonekana kuvutiwa na wachezajihao kutokana na viwango vyao, wakiwamo Pascal Wawa, Mussa Farid na wengineo wa Azam.
Mtu wa karibu na timu
hiyo wanayochezea Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu,
alisema kuwa mabosi wa TP Mazembe wamevutiwa na baadhi ya wachezaji wa
Yanga na Azam waliocheza Kagame wakipata picha kuwa Tanzania imesheheni
vipaji vya soka hivyo ni vema wakaelekeza nguvu zao ili kuviendeleza.
“Kombe la Kagame ni neema
kwa wachezaji wa Tanzania, (mabosi wa TP Mazembe) walikuwa wakifuatilia
sana mashindano hayo na kugundua vipaji vingi tu, wakiwamo Busungu,
Geoffrey, Deus Kaseke pamoja na wengine kutoka Azam, wakimtaja pia Wawa
raia wa Ivory Coast,” alisema mtoa habari wetu huyo ambaye hakutaka jina
lake kuwekwa hadharani.
Alisema TP Mazembe
wamebaini kuwa wanaweza kupata wachezaji wenye umri mdogo kutoka
Tanzania na kuwaendeleza kwa maslahi ya klabu yao kama wanavyonufaika na
akina Samatta na baadaye kuwauza Ulaya.
Uhamisho
wa Pedro kutoka FC Barcelona kwenda Manchester United uliripotiwa
kukamilika na walitakiwa kumalizana kila kitu wikiendi iliyomalizika
jana.
Kwa
mujibu wa Gazeti la Sport, sasa mambo yamebadilika, Barcelona
wamelazimika kuchelewesha kwasababu ya Neymar kupata majeruhi.
Mbrazil
huyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili za kwanza za msimu na hii
inamaanisha ataathiri safu ya ushambuliaji kuelekea mechi ya wiki hii ya
Super Cup dhidi ya Sevilla.
Kwasababu Pedro ni plan B ya Luis Enrique kumchezesha na Lionel Messi na Luis Suarez analazimika kubania kwa muda dili hilo.
Tovuti ya BCCSWAHILI Mwandishi wa habari za spoti amepigwa hadi kufa na mashabiki wa mchezaji aliyemkosoa katika ripoti yake.
Rasim
Aliyev raia wa Azerbaijan alimkashifu mchezaji nyota wa klabu ya Gabala
;Javid Huseynov, katika mtandao wa kijamii wa facebook.
Aliyev
aliandika '' Huseynov na timu ya kandanda ya Gabala wanapaswa kupigwa
marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya bara Ulaya kwa kupeperusha
bendera ya Uturuki
mbele ya mashabiki wa timu ya Cypriot inayotawaliwa na Ugiriki, Apollon Limassol.
Tukio hilo lilitokea baada ya mechi baina ya ya mchujo ya ligi kuu ya Europa mnamo Agosti tarehe 6.
Kufuatia ripoti hiyo Aliyev alipokea vitisho kadha dhidi ya maisha yake.
Dadake aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtu mmoja alimpigia simu na kutishia maisha yake.
Hatimaye alimpigia simu na kuomba wasameheane.
Inadaiwa kuwa Aliyev alikutana na mtu aliyedai kuwa binamu ya mshambulizi huyo akikusudia kuomba msamaha kwa maandishi yake.
Yamkini
mwandishi huyo alikuwa amekubali kukutana na mtu huyo kwa nia ya kwenda
kunywa chai naye kama ishara ya mapatano na uwiano lakini alipofika
sehemu waliokuwa wameahidi kukutana alivamiwa na kushambuliwa na
takriban watu 6 waliokuwa wamemuwekea mtego.
Alipigwa vibaya na akakimbizwa hospitalini.
Aliaga dunia jana alipokuwa akipokea matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali kuu ya Baku.
Hii si mara kwa Rasim kujipata taabani kufuatia uandishi wake.
Mwaka wa 2013,Rasim Aliyev alipigwa na maafisa wa polisi kutokana na ripoti yake.
Kichapo hicho kilinaswa kwa kamera na kuibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Azerbaijan