Tovuti ya BCCSWAHILI Mwandishi wa habari za spoti amepigwa hadi kufa na mashabiki wa mchezaji aliyemkosoa katika ripoti yake.
Rasim
Aliyev raia wa Azerbaijan alimkashifu mchezaji nyota wa klabu ya Gabala
;Javid Huseynov, katika mtandao wa kijamii wa facebook.
Aliyev
aliandika '' Huseynov na timu ya kandanda ya Gabala wanapaswa kupigwa
marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya bara Ulaya kwa kupeperusha
bendera ya Uturuki
mbele ya mashabiki wa timu ya Cypriot inayotawaliwa na Ugiriki, Apollon Limassol.
Tukio hilo lilitokea baada ya mechi baina ya ya mchujo ya ligi kuu ya Europa mnamo Agosti tarehe 6.
Kufuatia ripoti hiyo Aliyev alipokea vitisho kadha dhidi ya maisha yake.
Dadake aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtu mmoja alimpigia simu na kutishia maisha yake.
Hatimaye alimpigia simu na kuomba wasameheane.
Inadaiwa kuwa Aliyev alikutana na mtu aliyedai kuwa binamu ya mshambulizi huyo akikusudia kuomba msamaha kwa maandishi yake.
Yamkini
mwandishi huyo alikuwa amekubali kukutana na mtu huyo kwa nia ya kwenda
kunywa chai naye kama ishara ya mapatano na uwiano lakini alipofika
sehemu waliokuwa wameahidi kukutana alivamiwa na kushambuliwa na
takriban watu 6 waliokuwa wamemuwekea mtego.
Alipigwa vibaya na akakimbizwa hospitalini.
Aliaga dunia jana alipokuwa akipokea matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali kuu ya Baku.
Hii si mara kwa Rasim kujipata taabani kufuatia uandishi wake.
Mwaka wa 2013,Rasim Aliyev alipigwa na maafisa wa polisi kutokana na ripoti yake.
Kichapo hicho kilinaswa kwa kamera na kuibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Azerbaijan
No comments:
Post a Comment