Tuesday, September 8, 2015

ROONEY ALIA MACHOZI HUKU AKITOA UJUMBE KWA WENZAKE

Rooney 53Baada ya kuvunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya England kwa kufikisha magoli 50 hivi sasa, Wayne Rooney alijikuta mwenye hisia kubwa mbele ya wachezaji wenzake na mashabiki waliokuwa wakimpongeza mara baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 84.
Rooney mwenye miaka 29 alitokwa na machozi huku akinyoosha mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu kwa mafanikio aliyoyapata katika maisha yake ya soka.
Akiongea katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kuombwa kufanya hivyo na kocha Roy Hodgson, Wayne amesema ni wakati mkubwa na muhimu kwake na familia yake huku akiwapa changamoto vijana Raheem Sterling, Harry Kane na Ross Barkley kukomaa na kufikia hadi kupita rekodi yake siku zijazo.
Rooney 54Wachezaji lukuki wakiongozwa na David Beckham wamempongeza mchezaji huyo huku nahodha wa Chelsea, John Terry akienda mbali zaidi kwa kusema Rooney ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kuzaliwa England.
Chama cha soka England, FA kitamfanyia sherehe nahodha huyo wa England mwezi ujao katika mechi ya kufuzu itayofanyika Wembley katika usiku utakaoitwa Wayne Rooney ambapo atakabidhiwa kiatu cha dhahabu na Sir Bob Charlton ambaye ndiye alikua akishikilia rekodi hiyo kwa miaka 45 sasa.


JE UNAFAHAMU KWAMBA WAYNE ROONEY NI MFALME MPYA NCHINI ENGLAND

Rooney 50Jina la mchezaji Wayne Mark Rooney limekua gumzo nchini England wiki hii hasa pale ambapo alikua amebakiza goli moja tu kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya England, akimpita Sir Bob Charlton aliyeshikilia rekodi hiyo kwa kipindi cha miaka 45.

Wazza alifunga goli hilo la rekodi la 50 katika timu ya taifa na kumfanya sasa kuwa ni legendari wa England, heshima aliyoipata baada ya muda mrefu sana tangu akiwa na miaka 17 alipoibuka katika timu ya taifa.
Rooney 51Baada ya kufunga goli hilo la 50 dhidi ya Switzerland, mashabiki waliofurika katika uwanja wa Wembley waliripuka na kuimba, “Rooney! Rooney! Rooney!” huku Rooney mwenyewe akijikuta mwenye hisia kubwa baada ya kuweka historia hiyo.
Wachezaji mbalimbali wa zamani na sasa, kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameandika kumpongeza nahodha huyo mwenye miaka 29 kwa kuandika historia hiyo katika maisha yake ya soka.
Kocha wa England Roy Hodgson akimkabidhi Wayne Rooney jezi yenye namba ya magoli 50 ambayo Rooney ameifungia England na kuweka rekodi mpya
Kocha wa England Roy Hodgson akimkabidhi Wayne Rooney jezi yenye namba ya magoli 50 ambayo Rooney ameifungia England na kuweka rekodi mpya

JE UNAWAJUA MAGOLIKIPA 6 BORA DUNIANI? HAWA HAPA

Julio-Cesar
6. Julio Cesar-InterMilan (Brazil)
Tuzo binafsi
Kipa bora wa Serie A mwaka, 2008–09, 2009–10
Kipa bora wa UEFA mwaka : 2009–10
Kipa bora wa kombe la shirikisho mwaka 2013: 
FIFA Confederations Cup Dream Team: 2013
Primeira Liga Best Goalkeeper: 2014–15
 
5. Peter Shilton-Nottingham Forest (England)
Tuzo binafsi.
Kipa bora wa ligi daraja la kwanza mwaka: 1974–75, 1977–78, 1978–79, 1979–80, 1980–81, 1981–82, 1982–83, 1983–84, 1984–85, 1985–86
Mchezaji bora wa wachezaji mwaka: 1977–78
Mchezaji bora wa Nottingham Forest F.C. mwaka: 1981–82
Mchezaji bora wa Southampton F.C mwaka: 1984–85, 1985–86
4. Petr Czech-Chelsea,Arsenal (Jamhuri ya Cech)
Tuzo binafsi
Mchezaji bora wa UEFA Europa chini ya miaka 21: 2002 
Kipa bora wa Ligue 1: 2003–04
Timu bora ya mashindano ya UEFA Euro 2004
Kipa bora wa EPL : 2004–05, 2009–10, 2013–14 
Mchezaji bora wa EPL mwaka: 2004–05, 2013–14
Mchezaji bora wa Czech mwaka: 2005, 2008, 2009,2010, 2011, 2012, 2013 
Mpira wa dhahabu (Jamhuri ya Czech) : 2005, 2006, 2007, 2008, 2010, 2011, 2012, 2013
Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2005 
Kipa bora wa klabu katika michuano ya UEFA: 2005, 2007, 2008
Mchezaji bora wa wa mwezi wa Chama cha soka nchini Uingereza (FA) Premier League Player of the Month: March 2007
Mchezaji bora wa mwaka wa : 2010-11
3. Edwin Van der Sar-Manchester United (Uholanzi)
Tuzo binafsi 
Kipa bora wa mwaka Uholanzi: 1994, 1995, 1996, 1997
Mchezaji bora wa Ulaya : 1995, 2009
Timu ya mwaka ya ESM: 1995–96, 2008–09
Timu ya dunia ya All-Star: 1998 (Mchezaji wa Akiba)
Kiatu cha dhahabu nchini Uholanzi : 1998
Wawania kinyang’anyiro cha FIFA FIFPro World XI : 2006, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011
Alikuwepo kwenye kikosi bora cha EPL mwaka : 2006–07, 2008–09, 2010–11 
Mchezaji bora wa mechi michuano ya UEFA: Fainali 2007–08
Alikuwepo katika kikosi bora cha UEFA Euro 2008
Tuzo ya faida ya Barclays : 2008–09
Kipa bora wa EPL : 2008–09
UEFA Club Goalkeeper of the Year : 2009
 
2. Dino Zoff- Juventus (Italia)
Tuzo binafsi
Novemba 2003: Mchezaji bora wa Italy– Alikuwa ni mchezaji bora wa kizazi cha 50 iliyopita, ambapo alichaguliwa na Shirikisho la Soka Ulaya.
Mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or): 1973 (mshindi wa pili).
FIFA Order of Merit: 1984
UEFA European Championship Team of the Tournament: 1968, 1980
Timu ya wachezaji bora wa dunia wa UEFA: 1982
Kipa bora wa dunia wa FIFA: 1982
Tuzo ya mguu wa dhahabu ‘Golden Foot’ “Nguli wa soka”:2004
Mchezaji bora wa Italia “Hall of Fame': 2012
 
1. Manuel Neuer-Bayern Munich (Germany)
Tuzo binafsi 
Alipata tuzo ya medali ya fedha ya Fritz Walter kwa vijana chinya miaka 19 Silver 2005
Tuzo ya Silbernes Lorbeerblatt: 2010
Mchezaji bora wa Ujerumani mwaka: 2011,2014 
Alikuwepo timu ya mwaka ya ESM : 2011–12,2012–13 
Alikuwepo timu ya UEFA Euro mwaka : 2012 
Mchezaji bora wa fainali ya UEFA 2013 kwa upande wa mashabiki
Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2013, 2014
Kikosi bora cha FIFA/FIFPro : 2013,2014
Timu bora ya UEFA mwaka: 2013,2014 
Kikosi cha timu bora ya UEFA cha msimu wa: 2013–14 
Mchezaji bora wa pili wa UEFA: 2014 
Kipa bora wa kombe la dunia mwaka: 2014 
Alikuwepo kwenye kikosi bora cha ‘FIFA World Cup All-Star’ : 2014


-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif