Tuesday, September 8, 2015

JE UNAFAHAMU KWAMBA WAYNE ROONEY NI MFALME MPYA NCHINI ENGLAND

Rooney 50Jina la mchezaji Wayne Mark Rooney limekua gumzo nchini England wiki hii hasa pale ambapo alikua amebakiza goli moja tu kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya England, akimpita Sir Bob Charlton aliyeshikilia rekodi hiyo kwa kipindi cha miaka 45.

Wazza alifunga goli hilo la rekodi la 50 katika timu ya taifa na kumfanya sasa kuwa ni legendari wa England, heshima aliyoipata baada ya muda mrefu sana tangu akiwa na miaka 17 alipoibuka katika timu ya taifa.
Rooney 51Baada ya kufunga goli hilo la 50 dhidi ya Switzerland, mashabiki waliofurika katika uwanja wa Wembley waliripuka na kuimba, “Rooney! Rooney! Rooney!” huku Rooney mwenyewe akijikuta mwenye hisia kubwa baada ya kuweka historia hiyo.
Wachezaji mbalimbali wa zamani na sasa, kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameandika kumpongeza nahodha huyo mwenye miaka 29 kwa kuandika historia hiyo katika maisha yake ya soka.
Kocha wa England Roy Hodgson akimkabidhi Wayne Rooney jezi yenye namba ya magoli 50 ambayo Rooney ameifungia England na kuweka rekodi mpya
Kocha wa England Roy Hodgson akimkabidhi Wayne Rooney jezi yenye namba ya magoli 50 ambayo Rooney ameifungia England na kuweka rekodi mpya

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif