Tuesday, November 3, 2015

VANPERSIE NA DEPAY WATEMWA TEAM YA TAIFA

Van Persie + Depay
Memphis Depay na Robin Van Persie wametemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi cha hivi karibuni kwa kila mmoja kuwa na sababu zake zilizotajwa na kocha Danny Blind, baba wa mchezaji wa Manchester United, Delay Blind.
Kocha huyo amebainisha kuwa Memphis Depay (21) anahitaji kucheza kwa ajili ya timu zaidi ili apate nafasi katika kikosi hicho kwa maana sasa anaonekana hayupo tayari.
Aidha kuhusu mshambuliaji Robin Van Persie kocha huyo amesema, bado fomu na fitness ya Van Persie haiko sawa wakati huu na kwamba anahitaji kuangalia chipukizi katika nafasi hiyo ya ushambuliaji.
Uholanzi ilishindwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Ulaya EURO 2016 nchini Ufaransa huku wachezaji Robin Van Persie na Memphis Depay wakigombana wakiwa mazoezini kuelekea michezo hiyo ya kufuzu.
Depay aliyetarajiwa kuwa nyota mpya ya Uholanzi na hata kusajiliwa kwa dau la pauni milioni 25 kutoka PSV Eindhoven kuelekea Manchester United, amekua akifanya vibaya hadi kupelekea kuwekwa nje na kocha wake Louis Van Gaal wa Manchester United.


No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif