Saturday, November 19, 2016

Kauli za Mourinho na Wenger kuelekea mchezo wa Man United vs Arsenal jioni ya leo

azam-v-kageraLigi kuu ya England leo imerejea tena baada ya kupisha wiki ya michezo ya timu za taifa mbalimbali kwa mujibu wa kalenda ta Fifa duniani.
Urejeo wake umekuja na utamu wa aina yake pale jioni ya leo saa 9.45 utakaposhuhudiwa mchezo mkali kati ya Manchester United na Arsenal, mchezo utakaofanyika Old Trafford.
Mchezo unavuta hisia kali kutokana na uhasama uliopo kwa makocha wa timu hizi mbili, Jose Mourinho kwa upande wa Manchester United na Arsene Wenger kwa upande wa Arsenal.
Kuelekea mchezo huo, makocha wa timu zote mbili wamekuwa na maneno ya kusema huku kila mmoja akizungumza kwa maono yake juu ya mchezo huo.
kwa kuanza na meneja wa Manchester United Jose Mourinho, yeye anasema: “Rekodi yangu dhidi ya mameneja wa timu nyingine sio muhimu sana kwa leo. Kinachopatikana uwanjani inakuwa kwaajili ya timu.
“Mchezo wa leo ni kati ya mameneja wawili wenye rekodi bora kabisa kwenye Premier League. Sir Alex Ferguson hayupo hapa tena… nina mataji matatu hapa, vivyo hivyo kwa Arsene Wenger.
“Hiyo ina maana kwamba ni muhimu tuheshimiwe, hata pale matokeo yetu yanapokuwa si mazuri?
“Nadhani Wenger ana heshimu kwa ninyi nyote. Sidhani kama mimi ninayo, hasa kwa kuwa taji langu la mwisho la Premier League nimechukua miezi 18 iliyopita na sio miaka 18 iliyopita.”
Kwa upande wake, Arsene Wenger juu ya rekodi yake mbovu juu ya Mourinho: “Unajua, hatukuwa tukipoteza michezo yetu mara zote, tumewafunga lakini vilevile kumekuwa na michezo mingi tuliyomaliza kwa kutoshana nguvu.
“Nadhani nimepata ushindi dhidi ya meneja yeyote duniani katika kipindi cha miaka 20 niliyodumu hapa na sipo ktika mchezo huu kufanya ushindani kati ya mameneja wawili.
“Ni kati ya vilabu viwili na timu hizi mbili na nadhani naweza kuelewa kwamba watu wanataka kuleta utata, lakini hiyo si namna ya kuvuta hadhira. Kitakachovuta hadhira ni mvuto na ubora wa mchezo wenyewe.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif