Wednesday, November 2, 2016

LIVE KUTOKA SOKOINE MBEYA: MBEYA CITY 2 VS 1 YANGA (MPIRA UMEKWISHAAAAA)





MPIRA UMEKWISHAAA
-Mahundi kwa Mbeya City, anaingia Issa Nelson
-Mwashiuya anaachia shuti kali kabisa hapa, lakini nje.
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, kipa Mbeya City anaidaka krosi safi ya Msuva kwa ufundi kabisa
Dk 87, shuti kali la MWashiuya linapaaa juuuu ya lango la Mbeya City
Dk 86, Kessy anaingia vizuri na kuchonga krosi moto, City wanaokoa na kuwa konaaa, inachongwa na Mwashiuya, inaokolewa
Dk 81, bado inaonekana Mbeya City ndiyo wanaonekana kulalia kwenye lango la Yanga
DK 79, Nchimbi anawatoka mabeki wote wa Yanga, yeye na Dida anatoa nje
Dk 75, Niyonzima anaingia vizuri lakini Kenny Ally anamshitukia na kuokoa
SUB Dk 68, Yanga wanamtoa Tambwe na nafasi yake inachukuliwa na Obrey Chirwa
DK 64 sasa, mashambulizi ni kwa zamu na Mbeya City kidogo wanaongeza undava kidogo hasa upande wa walinzi na viungo wakabaji
Dk 59, Msuva anaachia shuti kali hapa lakini linamgonga beki na kuwa konaa, inachongwa haina manufaa
Dk 54, mpira umesimama, Mahundi wa Mbeya City anatibiwa
Dk 52, Niyonzima anawatoka mabeki wawili Mbeya City lakini wanaokoa na kuwa kona, hata hivyo haina matunda
SUB Dk 51, Yanga wanamtoa Kaseke aliyewahi kuichezea Mbeya City na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi kubwa na kupata kona, inachongwa hapa, shuti kali hapa lakini unatoka nje, goal kick...kipa wa Mbeya City yuko chini anatibiwa

MAPUMZIKO
GOOOOOOOO Ngoma anaunganisha krosi ya Msuva vizuri hapa na kuandika bao moja kwa Yanga

-KADI Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ally Ramadhani
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA 
Dk 44, hakuna matumaini kama Yanga wanaweza kusawazisha dhidi ya Mbeya City kwa kuwa hakuna shambulizi kali
Dk 42, mwamuzi anasema lile ni bao lililofungwa na Kenny Ally dak ya 36, hivyo Mbeya City wanaongoza kwa mabao 2-0

Dk 41 sasa, bado mpira umesimama na wachezaji Mbeya City wamekwenda kuwapumzisha mashabiki wao
Dk 35, Mbeya City wanaukwamisha mpira wavuni baada ya Kenny Ally kuukwamisha wavuni, Mwamuzi akaonyesha ni bao, halafu akabadilisha lakini mwamuzi anasema kuwa walicheza kabla ya filimbi. Mashabiki na wachezaji Mbeya City naona wanaonyesha hasira hapa, askari wanalazimika kuanza kuzuia vurugu hivi, mpira umesimama sasa
Dk 32, Raphael Alfa wa Mbeya City anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini Dida anaonyesha ujuzi na kupangua, kona. Yanga wanaokoa
Dk 28, Shamte anaachia 'bunduki' kali mpira wa adhabu, safari hii Dida anadaka kwa ustadi mkubwa
Dk 26, Msuva anaachia mkwaju safi hapa lakini kipa Mbeya City anapangua na kuwa konaaaa, inachongwa hakuna majibu mazuri
Dk 22, City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga

Dk 21, Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii
Dk 19, kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma
SUB Dk 19 upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani.
Dk 15, Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa

 Dk 14, Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili
Dk 13, Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda
Dk 11 sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha
GOOOOOOO Dk 6, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi

Dk 1, kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif