Monday, November 7, 2016

MAYANJA: HATUZIANGALII AZAM FC NA YANGA

Na Ram Mbegeze
Baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema wao hawaziangalii Yanga na Azam badala yake wanaangalia mwelekeo wao na mechi zao zijazo ambapo ameendelea kusisitiza kwao kila mechi ni fainali.
Mayanja alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu mwelekeo wa timu yao baada ya kupoteza mechi huku wapinzani wao wakipata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons na kupunguza pengo la pointi kutoka nane na kubaki pointi tano.
“Sisi hatuangalii Yanga wala Azam, tunaangalia mechi za Simba na kila mechi tunacheza kama fainali lakini kama matokeo yanakuja kama hivi ni bahati mbaya,” alisema Mayanja ambaye pia aliipongeza African Lyon kwa kupata matokeo ya ushindi.
Mayanja amesema walijaribu kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kubadili mfumo kwa ajili ya kutafuta ushindi lakini mambo yalikuwa magumu kwao kutokana na African Lyon kujaza mabeki katika eneo lao la ulinzi.
“Lyon walipaki basi, tulifanya kila kitu kubadilisha mfumo kwenda mbele kwa kuweka washambuliaji wanne lakini hatukufanikiwa. Siku haikuwa yetu wachezaji ni walewale ambao huwa tunawatumia kila siku na tunapata matokeo lakini haya ndio matokeo ya mpira.”

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif