Kutokana na story ya Samir NAsri kwamba Pep Gurdiaola amewapa ushari wachezaji wake kwamba wajihusishe na kukutana na wapenzi wao kabla ya usiku wa manane, imeibua hamu ya kujua maagizo mengine ya manager Pep ndani ya Etihad. Hivi hapa ni vitu sita ambavyo Pep ametoa maelekezo yake jinsi ya kufanyika ndani ya Etihad.
Sex
Pep huwa anasisitiza kwamba kitendo hiki kifanyike kabla ya usiku wa manane ili mchezaji apate muda mwingi wa kulala na kupumzika. Bila shaka hili hana uwezo wa ku-control zaidi ya kuwaamini wachezaji wake kwamba wanafuata anachokiagiza.
Pizza
Kuagizwa kwa Pizza kabla ya mechi ilikua ni kawaida kabla ya Pep hajaichukua timu. Lakini baada ya kuichukua Pizza haziruhusiwi kuja kabla ya mechi. Sasa hivi inameripitwa kwamba Pizzza huwa zinaletwa baada ya mechi ikiwa ni sehemu ya kurudisha nguvu baada ya mechi.
Breakfast
Ishu ya kuja na Sausage zako na mayai kwenye gari mazoezini kwa ajili ya chai mambo hayo hayapo ndani ya Etihad. Pep anatoa order kwa kila mtu kunywa chai au kula mezani pamoja kama familia zinavyofanyaga.
Juice za Matunda
Pep hataki wachezaji wake wanywe juisi za matunfa ambazo zina kiasi kikubwa cha sukari ambayo ni mbaya kwa afya yao. Pep hiwa ana sisitiza kwamba wachezaji wake wale matunda badala ya kunywa juisi iliyotengenezwa.
WiFi
Lengo kubwa anataka waongee wao kwa wao ili kuongeza kuzoeana nje ya uwanja. Kwenye eneo la kufanyia mazoezi simu zinakatazwa. Lakini Pep ameenda mbali zaidi kwa kuzuia WiFi kabisa ili kusiwe na connection yoyote.
Mitindo ya Nywere
Inasemekana kwamba Pep anakataza hadi wachezaji kujihusisha na style za nywere. Lengo lake anataka mchezaji a-focus kwenye mchezo zaidi ya kitu kingine chochote. Sasa angekua na mchezaji kama Pogba ingekuaje.
No comments:
Post a Comment