UEFA EUROPA LIGI itarindima Alhamisi Februari 19 kwa Mechi 16 za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na Uingereza ina Timu 4 kwenye hatua hiyo.
Timu hizo ni Everton, Liverpool, Tottenham za England na Celtic ya Scotland.
Liverpool, Tottenham na Celtic zote zitacheza Mechi zao za kwanza Nyumbani na Everton kukipiga Ugenini na Young Boys ya Uswisi.
Liverpool, ambao Msimu huu walianzia UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutupwa EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi lao, watakuwa kwao Anfield kuivaa Besiktas ya Uturuki bila ya Kiungo wao Chipukizi Lazar Markovic ambae amefungiwa Mechi 4 na UEFA.
Besiktas, wakiwa na Straika hatari Demba Ba chini ya Kocha mahiri Slaven Bilic wa Croatia, ni Timu ngumu inayocheza Soka la uwiano chini ya Mfumo 4-2-3-1.
Tottenham wao wapo kwao White Hart Lane kucheza na Fiorentina ya Italy wakati Cetic wao watakuwa huko Italy kucheza na Vigogo wa Nchi hiyo, Inter Milan.
+++++++++++++++++++++
MECHI ZA TIMU ZA UINGEREZA:
Young Boys v Everton
Liverpool v Besiktas
Tottenham v Fiorentina
Celtic v Inter Milan
+++++++++++++++++++++
Raundi hii itahusisha Mabingwa wa Nchi zao 7 pamoja na Timu mbili zilizowahi kutwaa Kombe hilo huko nyuma.
Aalborg BK (Denmark), AFC Ajax (Netherlands), RSC Anderlecht (Belgium), Celtic FC (Scotland), Legia Warszawa (Poland), Olympiacos FC (Greece) na FC Salzburg (Austria) ni Mabingwa Watetezi wa Nchi zao.
Sevilla FC ya Spain ndio Mabingwa Watetezi ambao pia walitwaa Kombe hili Mwaka 2006 na 2007 wakati VfL Borussia Mnchengladbach waliwahi kulibeba Mwaka 1974 na 1979.
Mabingwa Watetezi, Sevilla, wao wataanzia Nyumbani kucheza na WajerumaniBorussia Monchedgladbach.
Marudiano ya Raundi hii ni Wiki ijayo Alhamisi Februari 26.
UEFA EUROPA LIGI
RAUNDI YA MTOANO TIMU 32
Alhamisi Februari 19
**SAA 3 Usiku
Young Boys v Everton
Torino v Athletic Bilbao
Wolsfburg v Sporting Lisbon
Aalborg v Club Brugge
Dnipro v Olympiakos
Trabzonspor v Napoli
AS Roma v Feyernoord
PSV Eindhoven v Zenit St Petersburg
**SAA 5 Dakika 5 Usiku
Guingamp v Dynamo Kiev
Anderlecht v Dynamo Moscow
Ajax v Legia Warsaw
Sevilla v Borussia Monchedgladbach
Villarreal v FC Salzburg
Liverpool v Besiktas
Tottenham v Fiorentina
Celtic v Inter Milan
Alhamisi Februari 26
20:00 Zenit St. Petersburg v PSV Eindhoven
20:00 Dinamo Moscow v RSC Anderlecht
21:00 ACF Fiorentina v Tottenham Hotspur
21:00 Red Bull Salzburg v Villarreal CF
21:00 Besiktas v Liverpool
21:00 Internazionale v Celtic
21:00 FC Dinamo Kiev v Guingamp
21:00 Legia Warsaw v Ajax Amsterdam
21:00 Borussia Mnchengladbach v Sevilla FC
23:05 Club Brugge KV v Aalborg BK
23:05 Athletic de Bilbao v Torino FC
23:05 SSC Napoli v Trabzonspor
23:05 Olympiacos CFP v FC Dnipro Dnipropetrovsk
23:05 Sporting Lisbon v VfL Wolfsburg
23:05 Feyenoord Rotterdam v AS Roma
23:05 Everton FC v BSC Young Boys
Raundi zijazo
Raundi ya Mtoano Timu 16: Mechi 12 & 19 Machi
Robo Fainali: Mechi 16 & 23 Aprili
Nusu Fainali: Mechi 7 & 14 Mei
Fainali: Jumatano Mei 27, Tenth Anniversary Stadium, Warsaw, Poland
No comments:
Post a Comment