Nyota wa Simba SC Raphael Kiongera ameanza mazoezi mara moja mara baada ya jana kutua visiwani Zanzibar ambako Simba imekita kambi kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam FC utakaopigwa December 12, 2015 kwenye uwanja wa Taifa.
Kiongera amejiunga na Simba akitokea Kenya ambako alikuwa kwenye klabu ya KCB kwa mkopo mara baada ya kupona majeraha ya mguu yaliyomsumbua kwa muda mrefu.
Simba imeamua kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kufanya vizuri kwenye klabu ya KCB ambapo mwezi August mwaka huu alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi huo.
Kurejea kwake ni habari njema kwani Simba imekuwa ikimtegemea zaidi Hamisi Kiiza huku washambuliaji wengine wakioneka kutomshawishi kocha Dylan Kerr.
No comments:
Post a Comment