Siku
moja tu baada ya kuingia mkataba mpya na kampuni maarufu ya kuuza
matairi nchini ya Bin Slum Tyres, klabu uya Mbeya City imeanza kuonyesha
jeuri ya fedha.
Mbeya City imeingia mkataba na kiungo mshambuliaji kutoka Prisons ya Mbeya pia, mohammed Mkopi.
Mkopi
amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mbeya City ambayo imesaini
mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh milioni 300 kupitia bidhaa
za betri za magari za RB kutoka kwa Bin Slum.
Awali,
Mbeya City ilitaka kumchukua Didier Kavumbagu kutoka Azam FC, lakini
raia huyo wa Burundi aliamua kwenda nchini Vietnam ambako ameanza maisha
mapya ya soka.
No comments:
Post a Comment