Wakati
wowote kuanzia sasa Simba itamleta nchini straika Laudit Mavugo baada
ya kumaliza mkataba wake kuitumikia Vital’O ya Burundi baada ya awali
dili hilo kushindikana.
Tangu
mwaka jana, Simba ilikuwa ikimuwania Mavugo raia wa Burundi kila
kipindi cha usajili kinapofika lakini mambo huaribika na ikabidi isubiri
hadi straika huyo alipomaliza mkataba wake.
Mmoja
wa mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba ambaye hakutaka kutajwa jina,
amesema Mavugo atatua wakati wowote kuanzia sasa na tayari alisaini
mkataba wa miaka miwili tangu msimu uliopita.
Alisema
mkataba huo uliigharimu Simba Sh milioni 36, lakini awali walibanwa na
mambo ya mkataba wa straika huyo na timu yake hivyo kungoja hadi amalize
mkataba.
“Mavugo
atawasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa kuwa ni mchezaji wetu
na alisaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Simba na fedha
zilizotumika kwenye usajili wake ni Sh milioni 36.
“Kwa
sasa mkataba wake umekwisha kule katika timu yake aliyokuwa akiichezea,
hivyo yupo huru na ni uhakika atatua kuja kuichezea Simba msimu ujao,”
alisema bosi huyo.
Mavugo ana uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu na Simba inaamini atakuwa mkombozi wao msimu ujao na kuzima ngebe za wapinzani wao.
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment