Yanga
itakuwa dimbani Jumanne ijayo kuwavaa TP Mazembe katika mechi ya Kundi A
ya Kombe la Shirikisho Afrika linaloandaliwa na Shirikisho la Soka
Afrika (Caf) dhidi ya TP Mazembe, hofu kubwa ya timu hiyo ni beki ya
kushoto.
Wachezaji
wawili wanaocheza nafasi hiyo, Haji Mwinyi na Oscar Joshua wote wapo
katika hatari ya kuikosa mechi hiyo, hivyo Yanga ipo katika wakati mgumu
wa nani acheze nafasi hiyo.
Mwinyi
yeye ana kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo uliopita wa michuano
hiyo dhidi ya MO Bejaia ya Algeria wakati Joshua ana maumivu ya nyama
za paja, pia aliyapata katika mchezo huo.
Habari
njema kwa Yanga ni kwamba, Joshua tayari ameanza mazoezi mepesi kambini
huko mjini Antalya, Uturuki ambako timu hiyo imejichimbia kujiandaa na
mechi dhidi ya TP Mazembe.
Kutoka
Uturuki, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema: “Joshua anaendelea
vizuri na tayari ameanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mechi
na Mazembe.
“Bado
sijajua hatma yake kama atacheza au hatocheza mechi na Mazembe, hivyo
kila kitu kitajulikana ikiwa imebaki siku moja kabla ya mchezo wao baada
ya daktari wetu Edward Bavo kutoa ripoti yake.”
Joshua
alipata majeraha hayo usiku wa Jumapili iliyopita dakika ya 32 katika
mchezo dhidi ya MO Bejaia mjini Bejaia, Algeria ambapo ilibidi atolewe
na nafasi yake kuchukuliwa na Mwinyi. Katika mchezo huo, Yanga ilifungwa
bao 1-0.
No comments:
Post a Comment