Inawezekana kwenye orodha yako hukumuweka James Harden katika nafasi za juu sana kati ya wale wanaoweza kuwania tuzo ya mchezaji bora na mwenye thamani zaidi wa mwaka yaani MVP. Lakini kocha mpya Mike D’Antoni alikuwa anafikiri tofauti.
James Harden amekuwa akichezeshwa katika nafasi ya Point Guard na amekuwa akifanya vyema sana kiasi cha kuonyesha utofauti kuliko ilivyotegemewa hapo awali.
Nyota huyu wa Houston Rockets amejikuta akipata msaada mkubwa kwa wenzake na hii inamfanya kujiamini zaidi katika nafasi yake na majukumu yake mapya.
Harden alimaliza mchezo dhidi ya Washington Wizards akiwa na pointi 32 na assist 15 ukiwa ni mchezo wake wa nne akiwa na walau pointi 30 na assist 10 na kuiongoza Rockets kushinda 114-106 alfajiri ya leo.
Ryan Anderson alikuwa na pointi 23, Trevor Ariza aliongeza 15 na Clint Capela akamaliza mchezo akiwa na pointi 14.
John Wall wa Washington Wizard alivunja rekodi ya Wes Unseld na kuwa mchezaji aliyetoa assists nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo kabla hajaondolewa mchezoni zikiwa zimebaki sekunde 33.3 na timu yake ikiwa nyuma kwa pointi 5 na sasa wana rekodi mbovu ya 1-5.
Wall aliondolewa mchezoni akiwa na pointi 21 na assits 8.
No comments:
Post a Comment