KIKOSI CHA JKT MSIMU HUU |
Uongozi
wa timu ya Ruvu Shooting umesema kwamba, timu yao haiko tayari kucheza
mchezo wa ligi kuu kesho dhidi ya Yanga endapo Bodi ya Ligi/ TFF
watashikilia msimamo wao wa mchezo huo kuchezwa kesho katika uwanja wa
Uhuru, Dar es salaam.
Maamuzi
hayo yamefikiwa na uongozi wa timu chini ya Mwenyekiti wake Kanali
Charles Mbuge muda mfupi baada ya timu hiyo kuwasiri Mlandizi saa 4.15
asubuhi ya leo, Novemba 8,2016 ikitokea Kagera ambapo Jumapili
iliyopita, Novemba 6, 2016 ilicheza na Kagera sugar katika uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba.
Mwenyekiti
wa timu hiyo, Kanali Mbunge alisema, katika hali ya uchovu waliyonayo
wachezaji baada ya kusafiri safari ndefu ya zaidi ya KM 1450 kwa basi na
kutumia zaidi ya saa 22 kufika mwisho wa safari ni ajabu kufikia mchezo
mwingine wa ligi bila kupumzika japo kwa saa chache.
Kanali
Mbunge alisema, kuwapeleka wachezaji uwanjani kwa mazingira ya namna
hiyo, si tu kuwachosha bali ni kuwasababishia madhara makubwa kiafya
ambayo yanaweza kuwasababishia kifo, kwa hali hiyo akasisitiza
kutoipeleka timu uwanjani kesho kucheza na Yanga katika uwanja wa Uhuru,
Dar es salaam.
Aidha,
Kanali Mbunge alisema, mbali na madhara ya kiafya kwa wachezaji, mchezo
huo ukichezwa kesho, timu yake haitatoa ushindani wowote kwa timu
pinzani kwani, wachezaji wamechoka sana, miongoni mwao wakiwa ni
majeruhi ambao hawataweza kabisa kucheza mchezo huo kwa siku ya kesho.
Kanali
Mbunge alisema, kuliko kuwaua wachezaji kwa kuwafanyisha kazi ngumu
kama punda bila kupumzika, ni vema tupoteze pointi kwa kutopeleka timu
uwanjani, hao wapinzani wetu wapewe huo ushindi wa chee.
Awali
mchezo huo uliahirishwa kupisha mchezo wa Yanga wa Kimataifa na
kupangwa uchezwe Novemba 10, mchezo huo ulibadilishwa na kupangwa
uchezwe Novemba 11, baadaye ukabadilishwa tena ukapangwa Novemba 10,
hatimaye jana ukabadilishwa na kupangwa uchezwe Novemba 9.
Sijaona
sababu ya kuhairisha mechi hapa.c wanapata pesa za azma y hawapandi
ndege? Ulaya wanacheza jpili na jnne au jtano.wanacheza.
No comments:
Post a Comment