Winga Simon Msuva wa Young
Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya
Vodacom.
Msuva alikuwa na washindani
wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka
Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao
ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14
huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).
Kwa kushinda tuzo ya
mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka
kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment