Leicester City wamefudhu katika hatua ijayo ya Champions
League ambayo ni robo fainali baada ya kuitupa nje Sevilla, hakuna
aliyetarajia Leicester wanaweza kufika hapa walipo kutokana na kiwango
walichonacho msimu huu. Msimu huu Leicester wako na mwendo usioeleweka
kwani wanahangaika kupigania kubaki katika ligi kuu Uingereza, lakini
toka kocha aliyewapa ubingwa wa Uingereza Claudio Ranieri atimuliwe,
Leicester wanaonekana kurudi na makali mapyaa.
United nao katika mashindano ya Europa walipata suluhu ya moja kwa moja dhidi ya Rostov katika pambano lililopita, United watawakaribisha Rostov wiki hii wakiwa na faida ya goli la ugenini. Manchester United wanapewa nafasi kubwa kuchukua kombe la Europa katika msimu huu.
Sasa baasi katika timu nne za juu ligi ya Uingereza, Manchester United na Leicester hawapo.Chelsea anaongoza ligi, Totenham nafasi ya pili,Man City ya tatu na Liverpool ya nne na Arsenal ya tano. Katika Champions League timu tatu za juu ndizo zinafudhu moja kwa moja kushiriki Champions League lakini ligi moja inaweza kutoa timu tano.
Kama Leicester watabeba kombe la Champions League(bado mechi 4 kwa fainali) na United wakabeba Europa baasi aliyeko nafasi ya nne itabidi wampishe bingwa wa Europa, huku bingwa wa Champions League akienda kama bingwa mtetezi.
Hakuna aliyewaza kama Leicester wanaweza kuwa mabingwa wa Uingereza, vivyo hivyo watu wanawaza hawawezi kuwa mabingwa wa UEFA lakini wanaweza fanya lolote. Njia pekee ya Arsenal na Liverpool kujiweka mahali salama ili kucheza Champions League msimu ujao ni kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu.

No comments:
Post a Comment