Thursday, March 16, 2017

Tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo


Mtandao wa michezo wa Italia ujulikanao kama Tuttomercatto umeripoti kwamba, bosi wa Chelsea
anamuangalia kiungo wa Napoli Kalidou Koulibaly kama usajili wake wa kwanza katika dirisha lijalo la usajili. Conte amekuwa akimuwinda Msenegal huyo toka akiwa anaifundisha Juventus lakini sasa amemkazia buti na anataka kumchukua. Koulibaly ambae alisajiliwa na Napoli kutoka timu anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta timu ya Fc Genk, amekuwa na msimu mzuri sana toka awasili Napoli.
Tukibaki hapohapo katika klabu ya Chelsea, gazeti la Mirror linasema Chelsea wanajipanga kumchukua Romelo Lukaku kutoka Chelsea kwa dau kubwa sana. Lukaku ambaye amekataa kusaini mkataba mpya tena mnono na Everton ameanza kuwindwa na timu mbalimbali lakini Chelsea wanaonekana wako serious zaidi. Lukaku ambaye alikuwa Chelsea hapo mwanzo amekuwa na msimu mzuri sana safari hii na Chelsea wako tayari kuvunja account zao ili kumrudisha.
Sun nalo likiongelea usajili wa Lukaku kwenda Chelsea linasema, Chelsea wako tayari kumuuza Diego Costa ile endapo tu watafanikiwa kupata sahihi ya Lukaku na Alvaro Morata. Chelsea hawana uhakika wa kumbakisha Diego Costa msimu ujao, na kumekuwa na tetesi kwamba Costa anaweza kutimkia China au kurudi katika timu yake ya zamani ya Athletico Madrid.
Lakini vile vile kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yuko katika mbio za kumchukua mshambuliaji kinda wa RB Leipzig Timo Werner. Werner mwenye miaka 21 msimu huu amekuwa wa moto sana kiasi cha kuwatishia washambuliaji wa Bundesliga. Klopp anahitaji mshambuliaji mwingine wa kati na anamuona Werner kama mtu sahihi kwa Liverpool.
Neymar na Messi watofautiana kuhusu usajili, Neymar ni rafiki wa karibu sana wa Phillipe Coutinho na sasa Neymar amewaomba Barca wamnunue Coutinho toka Liverpool. Lakini Messi ni kama hataki Coutinho aje Barcelona. Messi anaona kama Coutinho akija Barcelona baasi itaharibu pacha yake ya ushambuliaji kati yake na Luis Suarez

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif