MKEMI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, LEO. |
Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu.
Simba
imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na
mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza
mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama
wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku
akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki
michuano ya Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka
Kombe la Dunia itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.
“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena.
”Watu
wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera
ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii
kesi.
“Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkem
No comments:
Post a Comment