Friday, April 14, 2017

GENK YA SAMATTA YAZIDIWA UJANJA NA CELTA VIGO, YACHAPWA 3-2 EUROPA LEAGUE



Celta Vigo ya Hispania imeanza vizuri hatua ya robo fainali ya Europa League kwa kuichapa KRC Genk ya Ubelgiji kwa mabao 3-2.
Mtanzania Mbwana Samatta alikuwa katika kikosi cha Genk na kuonyesha uwezo wa juu, lakini hakuweza kuisaidia kuimaliza Celta Vigo inayoshiriki La Liga.
Hata hivyo, Genk walicheza vizuri na kuonyesha wana uwezo wa kubadili matokeo katika mechi ya marudiano.
Genk ndiyo walitangulia kufunga bao kupitia kwa Jean Paul Boetius katika dakika ya 10 tu.
Wenyeji Celta Vigo wakacharuka na kupata bao katika dakika ya 15 kupitia Pione Sisto na mshambuliaji wao hatari, Iago Aspas akafunga la pili dakika ya 18.
John Guidetti akaongeza la tatu katika dakika ya 38 na Celta ikaenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 3-1.

Katika kipindi cha pili, Genk walikianza kasi na kufanikiwa kupata bao la dakika ya 67 na kuzidi kuufanya mchezo uwe mgumu zaidi.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif