Mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta (katikati) akiwatoka wachezaji wa Club America
Mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta (katikati) akiwatoka wachezaji wa Club America
Watanzania wanaokipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR wameshuhudia timu yao ikishindwa kupata ushindi kwa mara nyingine kwenye michuano ya FIFA Club Word Cup kufuatia kukubali kichapo kingine cha pili cha magoli 2-1 kutoka kwa Club America ya Mexico. Samatta na Ulimwengu wote walinza kwenye kikosi cha kwanza cha TP Mazembe dhidi Club America.
Magoli ya Dario Benedetto pamoja na Martin Zuniga yameipa America ushindi wa bao 2-1 dhidi ya TP Mazembe na kufanikiwa kuwa mshindi wa tano wa kwenye mashindano hayo mwaka 2015.
Mabingwa hao wa CONCACAF walichezea kichapo cha dakika za lala salama kutoka kwa Guangzhou Evergrande Taobao kwenye mchezo wao war obo fainali lakini shukrani zinaenda kwa Dario Benedetto na Martin Zuniga kwa kuisaidia timu yao kuibuka na ushindi.
Benedetto aliipa America bao la kuongoza dakika ya 20 kipindi cha kwanza na wakaongeza bao la pili kupitia Zuniga ambaye aliingia kipindi cha pili.
Rainford Kalaba aliifungia Mazembe bao la kufutia machozi kabla ya mapumziko lakini Club Amerika walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
Matokeo hayo yanaiacha TP Mazembe ikiwa nafasi ya sita ikiambulia dola za kimarekani milioni moja wakati Club Amerika yenyewe imefanikiwa kumaliza mashindano hayo ikiwa nafasi ya tano na kujinyakulia dola la kimarekani milioni moja na nusu.
Timu ya Auckland City baada ya kufungwa na Sanfrecce Hiroshima kwenye mchezo wa kwanza wenyewe moja kwa moja wanashika nafasi ya saba na kutokana na kushika nafasi hiyo wanajinyakulia kitita cha dola laki tano za kimarekani.