Wednesday, December 16, 2015

KAMUSOKO AIPELEKA YANGA KILELENI

Kiungo wa Mtakatifu Thabani Kamusoko
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Kamusoko
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Kamusoko ndiye aliyeibuka shujaa mkoani Tanga baada ya kuisadia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Sports ‘wanakimanu-manu’ wa jijini Tanga kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Iliwalazimu Yanga kupata bao dakika ya mwisho (90+5) kutokana na ugumu wa mchezo huo ambapo kwa muda wote Africans Sports walikuwa wamewabana Yanga vilivyo huku kila mtu akiamni mchezo huo utamalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mzimbabwe Thabani Kamusoko aliipatia Yanga bao safi akiunganisha kwa style ya ‘bicycle kick’ pasi ya kichwa iliyopigwa na mshambuliaji Donald Ngomba na kuipa Yanga pointi tatu muhimu.
Yanga ambayo ilibanwa mbavu na Mgambo JKT kwenye mchezo wa Jumamosi, imefanikiwa kukusanya pointi nne kwenye mkoa wa Tanga baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Mgambo ikajikuta ikiambulia pointi moja lakini leo imepata pointi tatu dhidi ya African Sports.
Matokeo hayo yanaifanya klabu hiyo ya Jangwani kufikisha ponti 27 baada ya kucheza michezo 11 na kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiiacha Azam ikiwa nafasi ya pili kwa ponti zake 26 ikiwa imecheza michezo 10.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif