Wednesday, December 16, 2015

UERO CLUB INDEX S YATABILI ARSENAL NDO BINGWA WA EPL MSIMU HUU

covvvv
Leicester ni club ambayo inafanya vizuri hivi sasa kwenye EPL ambapo imekua tishio kwa club kubwa kwenye mechi zao mbalimbali. Kama sio kutoka suluhu basi lazima washinde mechi dhidi yao.
Arsenal itachukua ubingwa EPL na Leicester itacheza UEFA msimu ujao ni ripoti kutoka ECI ambacho ni kirefu chake ni Euro Club Index. Hawa jamaa wametoa listi yao ambayo imetoa matokeo jinsi ligi ya EPL itakavyoisha.
Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Arsenal ndio itakua bingwa kwa msimu huu ikifuatiwa na Manchester City, Manchester United then Leicester City. Chelsea itamaliza kwenye nafasi ya 9 na Sunderland, Aston Villa na Norwich zitashuka daraja.
Concept ya ECI ili kupata matokeo haya ni kwamba wanatumia mechi za zamani za club hizo, performance ya wachezaji kwenye timu za taifa, mechi zao za sasa kwenye ligi na nyinginezo.
Mahesabu yao yanaendelea kuwa complicated sana hadi kufanya mahesabu ya mechi walizoshinda, walizofungwa hadi kwenye draw. Baada ya hapo wanachanganya na kupata matokeo kwa formula zao na ndio wakapata hii listi.
Mwisho wa siku mpira hauamuliwi kwa kutumia mahesabu ya kwenye karatasi bali kila kitu ni uwanjani. Huu hapa ni msimamo wa ligi jinsi ligi itakavyoisha kwa msimu huu
2F6CDF4700000578-3362345-image-m-47_1450276423863

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif