Aliyekuwa
mshambuliaji nyota wa Stand United, Elias Maguri amesaini mkataba wa
miaka mitatu wa kuitumikia Dhofar SC ya nchini Oman.
Maguri
ambaye alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita kabla hajaanza
kutoelewana na uongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, alisaini
mkataba huo jana.
Klabu
hiyo ndiyo wawakilishi wa Oman katika michuano ya Bara la Asia, hivyo
hii itampa Maguri nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa zaidi.
Awali
alikuwa akiwindwa na timu kadhaa ikiwemo Simba ya jijini Dar es Salaam
lakini alishindwa kujiunga nazo na kutimkia nchini Oman.
Kabla
ya kwenda kwenye timu hiyo, Maguri ambaye alitoka Simba kabla ya
kujiunga na Stand aliwahi kufanya majaribio kwenye timu ya TP Mazembe na
kusema kuwa amefanikiwa kufuzu, ingawa klabu yake ilimgomea kwa kuwa
hakufuata utaratibu wakati wa kwenda kwenye majaribio hayo.
Msimu
uliopita mshambuliaji wa huyo wa Taifa Stars, aliifungia timu yake
mabao 15 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Amissi Tambwe (21), na
Donald Ngoma (17).
No comments:
Post a Comment