Friday, November 25, 2016

Antoine Griezmann na safari ya kwenda Manchester.

screen-shot-2016-11-25-at-10-56-51-amMoja ya usajili ambao unasuburiwa kwa hamu na mashabiki wa Manchester united ni wa mchezaji Antoine Griezmann akitokea Atletico Madrid. Rais wa Atletico amesema hivi karibuni kwamba mchezaji wake hana mpango wa kwenda kokote zaidi ya kubaki hapo hapo kwenye club yake ya sasa.
Sasa connection na ushawishi wa club ya Manchester united unaendelea kuonekana hadi kwenye level za familia ya Griezmann. Antoine amekua bila wakala kwa muda sasa akiwa anategemea ushauri wa familia yake kudanya maamuzi yake ya kisoka.
Sasa kaka yake ameonyesha kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Manchester united hasa Wayne Rooney. Mapenzi hayo ameonyesha wakati Manchester wanacheza mechi dhidi ya Feyenoord. Theo Griezmann mtu wa karibu kabisa na Antoine alikua ana tweet live wakati mechi inaendelea akionekana kum-pusha Wayne Rooney aendelee kusukuma gozi uwanjani.
Moja ya tweet zake aliandika, “Come onnn!!!! ROONEY”. Kwenye tweet nyingine pia adhihirisha yeye ni shabiki wa Manchester kwa kuandika ,”Let’s go man united”.
screen-shot-2016-11-25-at-10-55-52-am
Baada ya tweet hizi jamaa ameanza kuwa maarufu huku mashabiki wa Manchester united wakimjibu tweet zake na kumwambia namba 7 ya Manchester united inamsubiri mdogo wake. Kwasababu Antoine anategemea ushauri wa karibu wa familia yake kwenye mambo yake ya soka. Inategemewa kwamba ushawishi wa kaka yake unaweza kuchangia star huyu kujiunga na kikosi cha O.T.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif