Kocha wa Stoke Mark Hughes ameelezea wasi wasi wake kwamba anaweza kumkosa mchezaji wake tena ikifika January. Pep alimruhusu Bony kusepa na kuanza ku-share mshahara wake wa £125,000 na Stoke city kwa wiki.
Dirisha la usajili linakaribia mwezi January na kuna kila dalili za Bony kuelekea China. Hughes amesema kwamba wameshakubali kwamba Stoke wanataka kumsajili kwa muda mrefu Bony lakini offer za China zinawapa wasi wasi.
Kutoka na hizo story za Bony kwenda china kocha alisema, “Kuna kitu cha ukweli kuhusu hili swala la Bony, mambo mengi yanatokea na ishu ya Bony kutaka kuondoka pia. Swala la yeye kuondoka kwenda huko lipo mikononi mwake.”
Kama Bony akihamia China atakua anaongeza idadi ya wachezaji wa Africa ambao wapo kwenye Super League ya China. Ligi hii inaonekana exclusive kwenye king’amuzi cha Startimes tu.
No comments:
Post a Comment