Kilichosubiriwa kimetimia na inawezekana kikawa. Kilichotegemewa pengine sicho kilichotimia, na kilifikiriwa inawezekana sicho kilichotokea. Wengi walisubiri kuona mchezo kati ya Oklahoma City Thunders dhidi ya Golden State Warriors hasa uhasama kati ya Kevin Durant dhidi ya Russell Westbrook.
Kevin Durant alihama kutoka klabu ya OKC na kuelekea Oakland katika klabu ya Warriors na ukawa ni uhamisho ambao ulizua maswali mengi ambayo wengi walihisi amekuwa mchezaji asiyejiamini na ambaye kama angehama hakutakiwa kujiunga na klabu yenye nyota wengine bali angeeenda kutengeneza ufalme wake mahali kwingine.
Alikwua ni Durant ambaye alikuwa na usiku mzuri zaidi kwani aliiongoza Warriors kupata ushindi mnono. Durant alipata mitupo 7 ya pointi 3 ambayo ndio mingi zaidi kuwahi kuipata katika mchezo mmoja na kumaliza mchezo na pointi 39. Warriors wakamaliza mchezo kwa kuichapa OKC na Russell Westbrook kwa pointi 122-96.
Westbrook alidhibitiwa na kufunga pointi 20 tu baada ya kuja katika mchezo huu akiwa mfungaji bora zaidi akiwa na wastani wa pointi 37.8 kwa mchezo.
Stephen Curry aliongeza pointi 21 points na assist 7, huku Klay Thompson ambaye amekuwa na msimu mbaya hasa kwenye ufungaji wake wa pointi 3 akifunga pointi 18, na kupata mitupo 4 ya pointi 3.
Victor Oladipo aliiongoza Oklahoma City akimaliza na pointi 21.
TAKWIMU
Kevin Durant amefunga pointi 20 au zaidi katika michezo 69 mfululizo akiungana na Michael Jordan ambaye alifanya hivyo kuanzia Nov. 24, 1990, mpaka April 19, 1991.
Pointi 39 za Kevin Durant zimekuwa pointi nyingi zaidi kwa mchezaji kuifunga timu yake ya zamani akilinagana na Danny Ainge na Stephon Marbury ambao waliwahi kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment