Mshambuliaji
hatari wa Athletic Bilbao, Aritz Aduriz ameonyesha umri si jambo baya
katika soka na una faida baada ya kufunga mabao yote matano wakati timu
yake ilipoimaliza KRC Genk ya Ubelgiji kwa mabao 5-3.
Ilikuwa
ni mechi ya Kombe la Europa na Mtanzania Mbwana Samatta alikuwa
uwanjani hadi Aduriz alipofunga bao lake la 4 katika dakika ya 74 na
akatika katika dakika ya 83.
Mechi
ilikuwa ngumu kwa kila upande Aduriz mwenye umri wa miaka 35
alipotupia bao katika dakika ya 8 na kuongeza tena katika dakika ya 24
lakini Genk wakajibu kwa kupata bao kupitia Leon Balley raia wa Jamaica.
Wakati
ikionekana kuwa mapumziko itakuwa 2-1, Aduriz alipachika tena bao
katika dakika ya 44 na kufanya hadi mapumziko iwe wenyeji wako mbele kwa
mabao 3-1.
Kipindi
cha pili, Genk walionekana wamepania baada ya kupata bao kupitia kiungo
wake Onyinye Ndidi na Aduriz akaongeza bao la nne katika dakika ya 74
na kuwavunja nguvu Genk.
Samatta
akitoka katika dakika ya 83 na kumuachia Nikos Karelis kumalizia dakika
saba zilizobaki lakini Aduriz akashindilia msumari wa mwisho katika
dakika ya 90.
No comments:
Post a Comment