Kocha Joseph Omog ameonyesha alivyo bora katika suala la saikolojia baada ya kuwaambia wachezaji wake, kazi haijaisha.
Omog
raia wa Cameroon, amesema waliweka nguvu kubwa kwa Stand United kwa
kuwa walijua ni timu ambayo haijapoteza mchezo kwenye Uwanja wa
Kambarage na tayari iliisha vifunga vigogo, Yanga na Azam FC.
“Kasema baada ya hapo, African Lyon ni timu nyingine ngumu. Wachezaji hatupaswi kufikiria kazi imeisha.
“Ule
mwendo ambao tumekuwa tukienda nao au tulioutumia dhidi ya Stand, dhidi
ya Lyon inabidi iwe zaidi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara na hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 13 ambayo wamecheza.
Leo wako Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza mechi yao ya 14.
No comments:
Post a Comment