Kiungo
wa Manchester City, Samir Nasri ambaye anakipiga Valencia kwa mkopo,
amesema kocha Pep Guardiola aliwakataza kufanya ngono baada ya saa sita
usiku.
Nasri
ameliambia gazeti namba moja la michezo la L’equipe la Ufaransa kwamba,
Guardiola aliwaambia baada ya saa sita usiku hakuna ngono kwa kuwa ni
hatari kwao.
“Alisema
ameweza kuwasaidia wachezaji kufanya vizuri kwa mfumo huo, alisema
Messi au Lewandowski walifanya vizuri kutokana na kupunguza kufanya
ngono baada ya saa sita.
“Alisema ukifanya hivyo unapata muda wa kutosha wa kupumzika na inasaidia sana,” alisema.
Nasri
raia wa Ufaransa aliondoka Man City katika hatua za mwisho za kufunga
dirisha baada ya kuona asingewezana na Mhispania huyo.
No comments:
Post a Comment