Akiwa bado hajafunga bao hata moja hadi sasa kwenye ligi ya England (EPL), striker wa Liverpool Daniel Sturridge huenda akaachana na kikosi cha Jurgen Klopp.
Alitupia kambani wakati England ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Scotland siku ya Ijumaa huku gazeti la The Mirror likiamini kwamba Sturridge yuko tayari kuachana na majogoo wa jiji ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
Kwa sasa Daniel Sturridge anapamabana kupata nafasi nyuma ya mbrazil Roberto Firmino pamoja mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi.
Inaripotiwa kuwa, Liverpool itahitaji kiasi cha pound milioni 28 kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji huyo aliyekulia kwenye academy ya Man City.
No comments:
Post a Comment