Na Baraka Mbolembole
GOLIKIPA namba moja wa Mwadui FC, Shaaban Kado amesema timu yao itanyanyuka na kuondoka chini ya msimamo katika ligi kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na mtandao huu mapema siku ya leo Jumanne, Kado amesema ni juhudi zitakazoambatana na matokeo mazuri ndizo zinahitajika katika kikosi chao ili kuondoka katika nafasi ya 14 waliyopo baada ya michezo 15 ya mzunguko wa kwanza kumalizika.
Timu hiyo ya Shinyanga imefanikiwa kukusanya pointi 13 tu, baada ya kushinda michezo mitatu, sare nne na kupoteza jumla ya michezo nane.
Wastani wao wa magoli ya kufunga na kufungwa ni wa kiwango cha chini mno kwani wamefunga magoli 12 tu na kuruhusu nyavu zao mara 21 (wastani wa magoli -9).
“Kila msimu ligi inakuwa ngumu kuliko ilivyokuwa misimu ya nyuma.” anasema, Kado mshindi mara mbili wa tuzo binafsi ya golikipa bora wa VPL (2008/09 na 2014/15.)
“Hatukuwa na matokeo mazuri sana katika raundi ya kwanza, na hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji wengi tegemeo kuondoka mara baada ya msimu uliopita kumalizika.”anaongeza Kado golilipa ambaye alidaka kwa kiwango cha juu katika game ya Taifa Stars vs Algeria miaka mitano iliyopita huko Algeria.
“Ili kujinasua katika nafasi za chini katika msimamo itatubidi kushinda tu mechi zetu. Tunajipanga kuhakikisha hilo linatimia.”
No comments:
Post a Comment