Friday, April 21, 2017

Nusu fainali UEFA ni kisasi cha Madrid, Monaco kinywani mwa Juventus.


Unakumbuka jinsi Simeone alivyofungwa na Real Madrid mara mbili katika fainali za Champions League? Pengine ni kati ya suala ambalo Simeone hataki kulikumbuka kabisa.
Lakini sasa amepewa nafasi ya kulipa kisasi kwani katika droo ya Champions League iliyofanyika mchana huu majirani hao wawili kutoka mji wa Madrid wanakutana katika nusu fainali ya Champions League
Atletico ambao walifika katika hatua hii baada ya kuwaondoa mabingwa wa soka wa nchini Uingereza klabu ya Leicester City wanakutana na Real Madrid ambao nao waliiondosha kwenye michuano hii miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.
Tayari watu wameshaanza kuusubiri mchezo huu kwa hamu kubwa haswa wakikumbuka fainali ya mwaka 2014 na ile ya 2016 ambazo ziliwakutanisha Madrid na Atletico huku zote Madrid wakiibuka kidedea
Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Monaco ambao msimu huu hawashikiki watakaokutana na timu ngumu zaidi kufungika katika mashindano haya ya msimu huu,klabu ya Juventus kutoka nchini Italia.
Monaco wanaingia katika nusu fainali hii wakijiamini kutokana na kuwa na safu ya ushambuliaji kiwembe ambapo Mbappe na Falcao wamekuwa wauaji wa nyavu lakini wakikutana na ukuta mgumu wa Juventus ambao waliwatoa Barcelona katika hatua ya robo fainali.
Nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 2 na 3 mwezi wa 5, kabla ya michezo ya marudiano itakayopigwa tarehe 9 na 10 ya mwezi huo huo wa tano.


No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif