Wakati bado wakiwa na
kumbukumbu ya kudhalilishwa nyumbani na mahasimu wao Barcelona, kisha
jana wakaondolewa kwenye michuano ya Copa Del Rey, leo hii kocha aliye
kwenye presha Rafael Benitez ataiongoza klabu yake ya Real Madrid
kuikaribisha Getafe Santiago Bernabeu.
Getafe ndio wageni wanaokaribishwa Bernabeu usiku wa leo na kwa namna hali ilivyo hakuna mjadala wa kuwazungumzia – kwa sababu Madrid wamekuwa wakiandamwa na sakata la kuondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya hukumu iliyotolewa jana – na leo mashabiki wa timu hiyo wanatarajia kuonyesha hasira zao kwa kocha Rafael Benitez kwa kile kinachoitwa uzembe wa kumpanga mchezaji ambaye alikuwa kafungiwa.
Madrid/Benitez wanaingia kwenye mchezo wa leo huku baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu wameonyesha nia ya kuchukua hatua za kisheria kwa klabu.
Katika mechi ya leo, James Rodriguez ambaye alikuwa kwenye ubora wake katika mechi vs Cadiz, anatarajia kuanza.
Jana ilitangazwa kwamba Benitez hakumuweka Marcelo katika kikosi cha mechi ya leo kutokana na majeruhi lakini cha kushangaza mchezaji huyo aliandika kwenye mitandao ya kijamii – “Nimepona kabisa na nipo tayari kucheza.” – jambo hili limezidi kuongeza sintofahamu baina ya Benitez na wachezaji wake.
Leo pia tunaweza kuona ‘BBC’ wakicheza kwa pamoja tena. Benzema alifunga magoli 6 katika mechi 6 za kwanza za ligi lakini akaumia na akaanza kuandamwa na kesi ya ulaghai dhidi ya Mathieu Valbuena – na sikza hivi karibuni amekuwa ‘off form’. Cristiano, kwa upande mwingine anaonekana kurudi kwenye mstari baada ya kufunga magoli matatu katika mechi 2 zilizopita. Usiku wa leo Ronaldo anakutana na timu ambayo ameshaifunga magoli 18 katika mechi 10 zilizopita – zikiwemo hat trick 3 na magoli mawili mawili mara 4.
Getafe hawana rekodi nzuri ugenini maimu huu – wameambuliwa kupata sare moja na magoli mawili tu katika mechi 6 zilizopita – rekodi mbaya zaidi ya ugenini kwenye La Liga. Leo usiku wa leo watakuwa bila Juan Rodríguez na hivyo wanategemewa kucheza kwa mfumo wa 4-1-4-1

No comments:
Post a Comment