Ujio wa Kocha Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United sasa ni gumzo na hofu kuu.
Tayari taarifa zinaeleza kwamba kama Mourinho atatua Manchester United, mara moja atamuuza kiungo Mhispania Juan Mata.
Taarifa
zinaeleza Mata aliyenunuliwa na Man United kwa kitita cha pauni million
37 kutoka Chelsea wakati huo Mourinho akiwa kocha, hata Marouane
Fellaini aliyenunuliwa kwa pauni million 27 kutoka Everton, naye safari
itamkuta.
Mata
na Mourinho hawakuwa katika uhusiano mzuri wakati kiungo huyo
alipoondoka Chelsea na kujiunga na Man United iliyokuwa ikifundishwa na
David Moyes.
Hali hiyo inazidisha hofu, kwamba Mourinho ambaye inaelezwa tayari amekubaliana na Man United kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.
Wachezaji hawana uhakika mani atabaki, mani ataondoka wakati kocha huyo atakapotua Old Trafford mwishoni mwa msimu.
No comments:
Post a Comment