McCarthy: Mourinho ndiye afaaye Man Utd
Jose Mourinho ndiye
afaaye zaidi kusaidia Manchester United kukabiliana vilivyo na
Manchester City watakaokuwa chini ya Pep Guardiola msimu ujao, haya kwa
mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Porto Benni McCarthy.
McCarthy, 38, alicheza chini ya Mourinho raia huyo wa Ureno alipokuwa mkufunzi wa Porto.
"Mourinho ni mmoja wa watu wanaojua jinsi ya kumshinda Guardiola na mbinu zake,” ameambia BBC Sport.
- Manchester United yazungumza na Mourinho
- Van Gaal akanusha uvumi kuhusu Mourinho
- Guardiola kuwa meneja Manchester City
"Kwa sasa sioni mtu yeyote anayeweza kumkabili Pep na mbinu zake Manchester City isipokuwa tu Mourinho akiwa United, atakwua na rasilimali, wachezaji na usaidizi wa kifedha wa kukabiliana na Guardiola."
Guardiola, alikuwa kocha wa Barcelona, kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City ilitangaza majuzi kwamba atamrithi Manuel Pellegrini majira yajayo ya joto.
Mourinho alifutwa kwa mara ya pili Chelsea mwezi Desemba, baada ya kushindwa mechi tisa kati ya 16 za kwanza ligini.
Alifutwa kazi miezi saba tu baada ya kuongoza klabu hiyo kushinda Ligi ya Premia.
Alikuwa Chelsea kwa kipindi cha kwanza 2004-2007.
No comments:
Post a Comment