Muda
mfupi baada ya taarifa kuzagaa kwamba boss wa Spurs Mauricio Pochettino
huenda akachukua kibarua cha ukocha kwenye klabu ya Manchester United,
tarari kuna taarifa zinazosema Jose Mourinho ameshamalizana na klabu
hiyo ya Old Trafford.
The
Sun linasema Man United wapo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa
manager wa Spurs lakini kiuhalisia inasemekana kocha huyo hana wakala.
Magazeti
matatu ya Jumatano (leo) yametoka na vichwa vya habari vinavyofanana
kila gazeti likidai Jose Mourinho ameshawaambia rafiki zake wa karibu
kwamba yeye ni kocha mpya wa Manchester United.
Tangu
kocha huyo atimuliwe na klabu yake ya zamani Chelsea, ripoti za
Mourinho kuchukua mikoba ya Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu
zimezagaa Ureno, Italia, Hispania na sasa England.
Jumapili
iliyopita Louis van Gaal alikuja juubaada ya kuulizwa kuhusu hatma yake
kunako Old Trafford baada ya Manchester United kuambulia sare ya
kufungana goli 1-1 dhidi ya Chelsea.
Hivi
ni vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti yaliyotoka leo huku habari
kubwa ambayo imepewa uzito na magazeti yote ni kuhusu Mourinho kutua Man
United.
P
No comments:
Post a Comment