Bayern Munich imeshinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bochum katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ujeurmani.
Shukurani
kwa mshambuliaji Robert Lewandowski aliyefunga mabao mawili yaani brace
na kusaidia kupunguza presha kwa kocha Pep Guardiola anayehamia Man
City.
Guardiola
amekuwa kwenye presha kubwa kutoka kwa magwiji wa Bayern ambao
wanaamini hawezi kukubaliana na timu nyingine suala la kuhamia kabla ya
kumalizana na klabu hiyo kwa maana ya kumaliza kazi zake.
Wanaamini hawezi kuwekeza akili zake zote Munich. Lakini ushindi huo, unazidi kupunguza presha hiyo.
No comments:
Post a Comment