ISHU YA KWENDA TP MAZEMBE, MAHADHI ASEMA KAMA VIPI POA TU
Kiungo
mshambuliaji mpya wa Yanga, Juma Mahadhi amefunguka kuwa yupo tayari
kujiunga na TP Mazembe iwapo watampa ofa ya maana huku akisisitiza
anajipanga kuisaidia timu yake katika michezo iliyobaki kwenye michuano
ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mahadhi
aliyejiunga na Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga, alionyesha uwezo
mkubwa katika mchezo dhidi ya TP Mazembe, Jumanne ya wiki hii kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar ambapo alidumu kwa dakika 65 kabla ya kubanwa na
misuli iliyosababisha atolewe na nafasi yake kuchukuliwa na Geoffrey
Mwashiuya.
Mahadhi
alisema kwa sasa anajipanga upya kwa ajili ya kuisadia timu yake katika
michezo iliyobakia ya michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa upande
wa ngazi ya klabu Afrika hivyo hataki kuipoteza nafasi hiyo.
“Ishu
kubwa ilikuwa ni misuli ilinikamata na kusababisha nishindwe kuendela
na mchezo japo awali nilikuwa nacheza kwa hofu sana, nikiogopa kuharibu
lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda nikawa naona kumbe naweza kufanya
kitu kwa ajili ya timu yangu ila bahati mbaya ndiyo hivyo sikuweza
kuendelea na mchezo ambao kwetu ulikuwa na umuhimu sana.
“Lakini naamini nitakuwa sawa mapema tu Mungu akipenda kwa sababu malengo yangu nimeyaweka katika michezo iliyosalia.
“Kama
Mazembe watakuwa kweli wananihitaji basi nitakuwa tayari kwenda
kujiunga nao iwapo wataleta ofa ambayo itakuwa na maslahi mazuri maana
mimi ni mchezaji na kazi yangi ni mpira sasa fursa ikitokea lazima
niitumie,” alisema Mahadhi.
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment