Baada
ya Klabu ya Simba kutangaza kutaka kumsajili straika Mrundi, Laudit
Mavugo, mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia,
nao wameingia kati wakiitaka saini ya straika huyo.
Simba
ambayo msimu uliopita ilimkosa Mavugo dakika za mwisho, tayari imeanza
mchakato wa kumnasa straika huyo huku ikitajwa Wekundu hao wa Msimbazi
wameweka mezani kitita cha dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 100).
Mtandao
wa Soka25east.com wa Kenya, umeripoti kuwa, Gor Mahia maarufu kwa jina
la K’Ogalo, ipo kwenye mikakati ya kumnasa Mavugo ambaye tayari
ametangaza kuondoka Vital’O ya Burundi.
Hata
hivyo, Rais wa Vital’O, Benjamin Bikorimana amesema bado anaamini
Mavugo ataendelea kuwepo klabuni hapo na kuipigania timu yake kuzidi
kupata mafanikio.
Wakati
huohuo, Mavugo amenukuliwa akisema: “Nataka kuondoka hapa Burundi na
kwenda kucheza soka la kulipwa kwani hiyo ndiyo ndoto yangu.”
Mavugo
ambaye aliwahi kuzichezea timu za Kiyovu, AS Kigali na Police FC, huu
ni msimu wake wa pili ndani ya Vital’O huku akiwa amefunga jumla ya
mabao 60 kwa kipindi chote hicho.
Upande
wa Simba kumekuwa na taarifa kuwa kuna uwezekano wa Mavugo kutua nchini
muda wowote kuanzia leo kwa kuwa wamefikia pazuri katika mazungumzo
yao.
No comments:
Post a Comment