Tukio
la shambulio la kigaidi kwenye Uwanja wa Ndege wa Ataturk mjini
Istanbul, Uturuki limebadili mipango ya Yanga kwenda kuweka kambi nchini
huko kubadilika na badala yake inajipanga kwenda Pemba.
Yanga
ilikuwa Antalya, Uturuki ilipoweka kambi kujiandaa na michezo yake
miwili ya Kombe la Shirikisho, ikaahidi kurejea Uturuki baada ya mechi
dhidi ya TP Mazembe, Jumanne ya wiki hii lakini sasa imebadili uamuzi.
"Timu
itaondoka kesho (leo) kuelekea Pemba kwa ajili ya kambi ya muda
kujiandaa na mechi na Medeama ambayo ni muhimu kwetu kupata ushindi ili
hesabu ziende sawa.
"Sisi
tulichopanga ni kushinda michezo yote iliyobaki ya Kombe la Shirikisho
Afrika baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya MO Bejaia na Medeama.
"Maamuzi
hayo ya kambi ya Pemba yametokana na tukio kubwa la kigaidi
lililofanywa huko Uturuki, hivyo kiusalama tumeona ni vema tukabaki
nchini," alisema mtoa taarifa wetu.
Alipotafutwa
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
kuzungumzia hilo alisema: "Kambi yetu tutaitangaza wakati wowote wapi
tutakapokwenda, hivyo subirieni kwanza tutawajulisha.”
No comments:
Post a Comment