Tuesday, October 25, 2016

YANGA KUFUMUA BENCHI LA UFUNDI LA TAIFA STARS, WA KWANZA MKWASA



Kocha Charles Boniface Mkwasa yuko katika rada za Yanga na tayari wamefanya mazungumzo naye.

Mkwasa amezungumza na Yanga kuhusiana na suala la kurejea kuchukua nafasi ya kocha msaidizi.

Taarifa za ndani za Yanga, zinaeleza Mkwasa anaonekana kuwa mkali na anayetaka kufanya mambo yake kwa uahakika.

“Mkwasa ni mkali, kocha msaidizi anatakiwa kuwa ni yule ambaye hataki mchezo. Hivyo uongozi wa Yanga unaonekana kutaka kumrejesha.

“Umezungumza naye mara mbili na inawezekana kweli akarejea,” kilieleza chanzo.

Pamoja na Mkwasa, mwingine anayeweza kutua Yanga katika benchi jipya la ufundi ni Manyika Peter, kipa wa zamani wa timu hiyo ambaye amekuwa akifanya kazi na Mkwasa katika kikosi cha timu ya taifa.

Pia kiungo wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua anapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya meneje, Hafidhi Saleh.

Uamuzi wa Yanga unafuatia kubadilishwa kwa Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm na kumchukua George Lwandamina wakati Yanga ikiwa ndio imeanza kuamka.

WANDAMINA AREJEA ZAKE ZAMBIA BILA YA KUSAINI MKATABA YANGA


Kocha George Lwandamina amemalizana na Yanga kwa maana ya mazungumzo lakini amerejea nchini mwao bila ya kusaini mkataba na Yanga.

Kocha huyo ameondoka nchini leo alfajiri kurejea Lusaka Zambia kwa ajili ya kumalizia mambo ya kifamilia.

“Baada ya hapo atarejea na kusaini mkataba, utakuwa ni wa miaka miwili nimeelezwa,” kilisema chanzo.

Lwandamina ndiye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi.


Kocha huyo wa zamani wa Zesco, alitua nchini juzi na kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga.

BAADA YA MIEZI NANE, HATIMAYE ZOUMA AREJEA UWANJANI NA KUITUMIKIA CHELSEA

Beki Kurt Zouma amerejea uwanjani na kuichezea Chelsea kwa mara ya kwanza miezi nane.

Zouma aria wa Ufaransa alivunjika mguu upande wa viunganishi via mguu lakini jana ameichezea Chelsea akikitumikia kikosi cha vijana chino ya miaka 23.

Katika kikosi hicho, Zouma mwenye umri wa miaka 21, alicheza vizuri katika mechi hiyo dhidi ya Derby County na kuonyesha sasa yuko safi.


Daktari alitaka acheze kwa dakika 45 tu, kweli akafanikiwa. Maana yake baada ya hapo atakuwa chini ya uangalizi huku akijiandaa kurejea katika kikosi cha Kocha Antonio Conte.

Yanga imemtangaza C.E.O atakaeanza kazi November 19



Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga imemteuwa Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu kuendesha klabu pamoja na kusimamia fedha.
Mfaransa huyo ambaye amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka la Rwanda (Ferwafa) pamoja na FC Talanta ya Kenya amepewa jukumu la kuhakikisha klabu inapata mafanikio barani Afrika.
Lengo langu kuu itakuwa ni kutekeleza vipaumbele vya klabu ikiwemo kuweka misingi ya kujenga soka la vijana kwa kuanzisha vituo vya kukuza vijana wadogo, kujenga viwanja vya nyasi bandia na kutafuta mapato kwa ajili ya hilo,” Dufourg aliimambia supersport.com alipofanyiwa mahojiano maalum.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajia kutua Dar wiki ijayo apambapo ataanza rasmi kutekeleza majukumu yake November 19.
Mwenyekiti wa Yanga na mfanyabisha maarufu nchini Yusuf  Manji anataka kuijenga klabu ya Yanga kuwa miaongoni mwa vilabu vyenye uwezo barani Afrika na anaamini uteuzi wa Dufourg utaisaidia Yanga kufikia malengo.
Inatajwa kuwa, mwaka uliopita mapato ya Yanga yalikuwa ni doka za kimarekani 593,865 sawa na shilingi bilioni 1.3 za kitanzania huku matumizi yakiwa ni dola za kimarekani milioni 1.3 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 2.88 za kitanzania hivyo klabu kuendeshwa kwa hasara lakini Manji anataka Yanga iendeshwe kwa faida.
Kuhusu Mamelodi Sundowns inayoshiriki ligi ya soka ya Afrika Kusini (PSL) kufanikiwa tutwaa ubingwa wa vilabu barani Afrika (Caf Champions League), Dufourg amesema: “Mamelodi Sundowns wameonesha kuwa mipango na maandalizi mazuri yanavyosaidia mataji kitu ambacho tunatakiwa kujifunza, kujenga vilabu vyenye uwezo kama TP Mazembe ya DR Congo na Mamelodi Sundowns.”

Xavi atupa dongo kwa Mourinho

1Kiungo na nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez amemuelezea meneja wa Manchester Jose Mourinho kama mtu mwenye kupenda vita kuliko soka pale ambapo mambo hayamwendei sawa.
Ni hivi karibuni tu baada ya mchezo wa Chelsea na Man United ambao uliisha kwa United kupigwa 4-0, Mourinho alimshambulia Conte kwa kumwambia anashangilia kupita kiasi.
Hili ni tukio ambalo lilikuja baada ya Mourinho kukwaruzana na Jurgen Klopp, kitu ambacho kocha huyo wa Liverpool alikiita ni cha kipuuzi.
Na sasa Xavi naye amekuja na maoni yake na kusema kuwa, meneja huyo huwa anashindwa kuendana na mambo yanapokuja kinyume na matarajio yake na kuongeza kuwa anapaswa kuachana na kugombana makocha wenzake.
“Wakati mwingine, wakati mambo yanapokwenda kinyume na Mourinho, anapenda zaidi vita kuliko soka, kama wakati ule alipokuwa Real Madrid, na naamini hayo hatutayaona tena England,” Xavi amesema.
Mourinho amekuwa kwenye presha kubwa kwenye klabu ya ManchesterUnited kufuatia mwenendo usioridhisha a timu hiyo.


-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif