Tuesday, October 25, 2016

Xavi atupa dongo kwa Mourinho

1Kiungo na nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez amemuelezea meneja wa Manchester Jose Mourinho kama mtu mwenye kupenda vita kuliko soka pale ambapo mambo hayamwendei sawa.
Ni hivi karibuni tu baada ya mchezo wa Chelsea na Man United ambao uliisha kwa United kupigwa 4-0, Mourinho alimshambulia Conte kwa kumwambia anashangilia kupita kiasi.
Hili ni tukio ambalo lilikuja baada ya Mourinho kukwaruzana na Jurgen Klopp, kitu ambacho kocha huyo wa Liverpool alikiita ni cha kipuuzi.
Na sasa Xavi naye amekuja na maoni yake na kusema kuwa, meneja huyo huwa anashindwa kuendana na mambo yanapokuja kinyume na matarajio yake na kuongeza kuwa anapaswa kuachana na kugombana makocha wenzake.
“Wakati mwingine, wakati mambo yanapokwenda kinyume na Mourinho, anapenda zaidi vita kuliko soka, kama wakati ule alipokuwa Real Madrid, na naamini hayo hatutayaona tena England,” Xavi amesema.
Mourinho amekuwa kwenye presha kubwa kwenye klabu ya ManchesterUnited kufuatia mwenendo usioridhisha a timu hiyo.


No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif