Kocha
George Lwandamina amemalizana na Yanga kwa maana ya mazungumzo lakini
amerejea nchini mwao bila ya kusaini mkataba na Yanga.
Kocha huyo ameondoka nchini leo alfajiri kurejea Lusaka Zambia kwa ajili ya kumalizia mambo ya kifamilia.
“Baada ya hapo atarejea na kusaini mkataba, utakuwa ni wa miaka miwili nimeelezwa,” kilisema chanzo.
Lwandamina ndiye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi.
Kocha huyo wa zamani wa Zesco, alitua nchini juzi na kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga.
No comments:
Post a Comment