Tuesday, October 25, 2016

Yanga imemtangaza C.E.O atakaeanza kazi November 19



Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga imemteuwa Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu kuendesha klabu pamoja na kusimamia fedha.
Mfaransa huyo ambaye amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka la Rwanda (Ferwafa) pamoja na FC Talanta ya Kenya amepewa jukumu la kuhakikisha klabu inapata mafanikio barani Afrika.
Lengo langu kuu itakuwa ni kutekeleza vipaumbele vya klabu ikiwemo kuweka misingi ya kujenga soka la vijana kwa kuanzisha vituo vya kukuza vijana wadogo, kujenga viwanja vya nyasi bandia na kutafuta mapato kwa ajili ya hilo,” Dufourg aliimambia supersport.com alipofanyiwa mahojiano maalum.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajia kutua Dar wiki ijayo apambapo ataanza rasmi kutekeleza majukumu yake November 19.
Mwenyekiti wa Yanga na mfanyabisha maarufu nchini Yusuf  Manji anataka kuijenga klabu ya Yanga kuwa miaongoni mwa vilabu vyenye uwezo barani Afrika na anaamini uteuzi wa Dufourg utaisaidia Yanga kufikia malengo.
Inatajwa kuwa, mwaka uliopita mapato ya Yanga yalikuwa ni doka za kimarekani 593,865 sawa na shilingi bilioni 1.3 za kitanzania huku matumizi yakiwa ni dola za kimarekani milioni 1.3 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 2.88 za kitanzania hivyo klabu kuendeshwa kwa hasara lakini Manji anataka Yanga iendeshwe kwa faida.
Kuhusu Mamelodi Sundowns inayoshiriki ligi ya soka ya Afrika Kusini (PSL) kufanikiwa tutwaa ubingwa wa vilabu barani Afrika (Caf Champions League), Dufourg amesema: “Mamelodi Sundowns wameonesha kuwa mipango na maandalizi mazuri yanavyosaidia mataji kitu ambacho tunatakiwa kujifunza, kujenga vilabu vyenye uwezo kama TP Mazembe ya DR Congo na Mamelodi Sundowns.”

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif