Ushindi
wa mabao 2-1 walioupata Mbeya City dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi
Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana unakuwa mtihani
mwingine kwa Yanga.
Yanga wanaingia kwenye mtihani huo kutokana na mechi inayofuatia dhidi ya Prisons ambao wanakutana nao Jumamosi.
Prisons ambao wanashindana kwa juhudi zote na Mbeya City, hawatakubali kuona wao wanaishindwa Yanga kwa mambo mawili.
Kwanza ni kwa ajili ushindani wao mkali dhidi ya Mbeya City ambao wamewaonyesha wamewaweza Yanga, vipi wao washindwe?
Pili
wanachuana na Mbeya City kwa pointi, Prisons sasa wana 16 na
wasingependa kuzidiwa zaidi kwa kuwa sasa tayari Mbeya City wana 19.
Kufanikisha
yote haya, lazima Prisons washinde ili kuwakimbiza wapinzani wao Mbeya
City, pia kuwaonyesha hakuna wanachoshindwa pia.
.
No comments:
Post a Comment