Mshambuliaji wa klabu ya arsenal, Alexis Sanchez anashutumiwa kuhusika na ubadhikifu wa fedha zinazosimamiwa na mamlaka ya kodi ya Hispania inayokadiriwa kuwa kiasi cha Euro Milioni moja (€1 million) kutokana na kile kilichopatikana kwenye haki za sura yake akiwa na klabu ya Barcelona, hii imetajwa na gazeti la Katalunya, El Periodico.
Jarida hilo la kila siku limeripoti kuwa mamlaka ya mashitaka na kesi za jinai imefungua kesi ya madai dhidi ya Sanchez ambaye anadaiwa kukwepa kulipa kodi ya mapato katika kipindi cha miaka 2012 na 2013 kinachokadiriwa kuwa €983,443 (£889,169) ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania 2392779271, bilioni mbili na milioni 400.
El Periodico limesema kuwa Sanchez, ambaye alijiunga na Arsenal katika majira ya joto ya mwaka 2014 baada ya misimu mitatu akiwa Barca, inasemekana alitumia makampuni kutoka Chile na yale ya Malta kusimamia upatikanaji wa fedha zake za mauzo ya sura yake.
Ripoti ya jarida hilo inasema kuwa mchezaji huyo raia wa Chile anadaiwa kufanya ubadhilifu wa kiasi cha fedha za kitanzania bilioni moja na milioni mia tano, 1581455655 (€587,677) mwaka 2012 na bilioni moja na milioni 60, 1065017652 (€395,766) mwaka 2013.
Kama ikithibitishwa, Sanchez mwenye miaka 29 atakuwa mchezaji wa tano kutoka katika vitabu vya klabu ya Barcelona kuhusishwa na tatizo la fedha na mamlaka za mapato katika mahakama za Hispania.
Mapema mwaka huu, nyota wa Barcelona Lionel Messi alikutwa na hatia kwa makosa matatu ya ubadhilifu fedha na mahakama za nchini humo. Messi alipiwa faini pamoja na adhabu ya kifungo cha miezi 21 jela.
Alexis Sanchez aliichezea Barcelona katika kipindi cha miaka ya 2011 na 2014.
Mchezaji mwenzie na Messi katika klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Javier Mascherano alikutwa pia na hatia ya mauzo ya haki za sura yake na akahukumiwa pia kulipa faini na kifungo cha mwaka mmoja.
Nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o, aliyeichezea Barca kuanzia mwaka 2004 na 2009 ambaye kwa sasa yupo na klabu ya Uturuki, Antalyaspor, na pia raia wa Brazil beki Adriano wote wamewahi kukutwa na kesi za ukwepaji kodi nchini Hispania.
No comments:
Post a Comment