Monday, November 14, 2016

Cleveland Hawakamatiki ni shidaaa


cleveland-cavs_96lhgpxyii5j13cyjb0quoo5f
LeBron James hakumuhitaji Kevin Love au Kyrie Irving ili kumaliza mchezo dhidi ya Charlotte Hornets na hii hutokea kwa vilabu vichache ambavyo wachezaji wake wanaaminiana.
James,alikuwa ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza katika robo ya nne ya mchezo huo, akafunga pointi 11 kati ya pointi zake 19 katika kipindi cha mwisho na kuisadia Cavaliers kuibuka na ushindi wa pointi 100-93 dhidi ya Charlotte Hornets.
Channing Frye akafunga pointi 20 ambazo ni nyingi zaidi kwake msimu huu huku pia akicheza dakika zote za robo ya nne akiwa pamoja na James, Iman Shumpert, Richard Jefferson na Jordan McRae.
Kyrie Irving aliongeza pointi 19 huku Kevin Love akiendelea kuwa na kiwango bora na alimaliza mchezo akiwa na pointi 17, katika mchezo ambao alikosekana J.R. Smith, kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.
Cleveland Cavalierswameweka rekodi ya kupata walau mitupo 10 ya pointi 3 katika michezo 9 ya kwanza ya msimu.
Kemba Walker alifunga pointi 21 kwa upande wa Hornets, ambao wamepoteza michezo miwili mfululizo baada ya kuanza ligi vyema kwa rekodi ya 6-1.

No comments:

Post a Comment

-------------------------------------------------------

-------------------------------------------------------
HABARI MPYAMPYAhttp://2.bp.blogspot.com/-mFnDPXvIysA/VOZH1z-2rpI/AAAAAAAAADs/shOR30FtkF4/s1600/anigif.gif